• Thursday, November 26, 2026

Mpendwa mteja,

NETPOA imehamia eneo jipya la wateja: https://my.netpoa.com. Akaunti yako, huduma, domain na historia ya ankara zimehamishiwa huko.

Jinsi ya kuingia mara ya kwanza

  1. Nenda https://my.netpoa.com/forgot-password
  2. Weka barua pepe unayotumia kwetu.
  3. Fungua barua pepe tutakayokutumia na uweke nenosiri jipya.

Utafanya hivi mara moja tu. Nenosiri lako la zamani la tovuti hii halitafanya kazi huko.

Kinachobadilika

  • Ankara za kuhuisha huduma sasa zitatoka my.netpoa.com. Unaweza kulipa huko kwa pesa ya simu au kadi.
  • Salio lolote ulilonalo litahamia pamoja nawe.
  • Tiketi za msaada, DNS, kuingia kwenye hosting na usimamizi wa domain vyote viko kwenye eneo jipya.

Wauzaji wa domain (resellers)
Akaunti yako ya reseller, salio na domain zako sasa ziko my.netpoa.com. Utapokea barua pepe yenye API key mpya. API secret inaonyeshwa mara moja tu kwenye paneli yako ya reseller: inakili kutoka hapo na uweke kwenye mipangilio ya module yako ya WHMCS. Funguo za zamani hazifanyi kazi tena.

Tovuti hii itaacha kupokea malipo hivi karibuni. Tafadhali ingia my.netpoa.com na uangalie huduma zako.

Unahitaji msaada? Wasiliana nasi WhatsApp 0755212222

Asante kwa kuendelea kuwa nasi.