NetPoa

Your Online Partner

Masharti

netpoa.com ni zao la NetPoa Limited ambayo inahusika na Kutengeneza Website, Website Hosting, Domain Registrations, na Internet Marketing, ndani ya Tanzania tangu mwaka 2017. Kwa kutumia huduma zetu basi utatakiwa uwe umekubaliana na sera za faragha, masharti na vigezo ambavyo tumetoa kama ifuatavyo;

Sera za Faragha:

Tutakusanya taarifa zako kama Majina yako, jina la biashara yako, namba za simu, barua pepe, mahali unapoishi kwa lengo kuu la usajili wa domain name, kuweka taarifa hizi kwenye website yako na kwa ajili ya mawasiliano yetu na wewe.

Taarifa zozote unazotupatia zinabakia kwetu pekee hatusambazi kwa mtu mwingine yeyote.

Tunatumia mfumo wa WordPress katika kutengeneza Website zetu hivyo kwa mfumo huu na wao watakuwa na baadhi ya taarifa zako ni muhimu kutambua hili. WordPress pia inakuwa na plugin mbalimbali ambazo hutumika katika kutengenezea website nazo kuna baadhi zinaweza kutumika katika kukusanya taarifa.

Kama kutakuwa na tatizo lolote kuhusiana na mfumo wetu tunaoutumia tutakutaarifu mapema ili uweze kulinda taarifa zako.

Malipo:

Tunapokea malipo kwa njia ya simu.

Tunapokea malipo kuanzia Miezi sita na Mwaka mmoja kwa huduma ya Web hosting. Kwa website designing na domain gharama zote hulipwa mara moja.

Utahitajika kulipia (renew) huduma yako mapema kabla muda haujakwisha kwasababu kufanya hivyo kutasababisha Website yako au domain isiwepo hewani. Unashauriwa kulipia siku kumi kabla ili kuepuka usumbufu wa website yako kuondoka hewani.

Huduma ambazo zinafanyiwa renew kila mwaka ni Hosting na Domain.

Tutakukumbusha kwa njia ya barua pepe, na simu siku kumi kabla ya website na domain yako haijakaribia kuisha muda wake wa kuwa hewani.

Endapo utashindwa kulipia kwa wakati tutakaa na data zako kwa muda wa siku 7 tu baada ya hapo zitaondolewa kwenye server zetu na hivyo itakugharimu zaidi iwapo utazihitaji tena.

Matengenezo:

Kwa huduma ya Web Design matengenezo yake huchukua siku 3- 7 kulingana na ukubwa wa kazi ambayo umetupatia.

Web Hosting SetUp huchukua kuanzia lisaa limoja hadi masaa 24, hii ni kwasababu domain name inaponunuliwa kuna hatua hupitia hivyo wakati mwingine inaweza kuwahi kuwa active na wakati mwingine huchelewa. Ni vyema ukafahamu hili.:

Maboresho (Updating)

Unaweza kuwa unahitaji kuweka taarifa mpya kwenye website yako baada taarifa za zamani kupitwa na wakati au tu umekuwa na huduma mpya unataka kuziongeza kwenye website yako. NetPoa tutakufanyia kazi hii kwa gharama nafuu sana ya Tsh 10,000/= (elfu kumi tu) hivyo usiwe na wasiwasi wakati wowote.

Karibu Sana.