KILA SIKU UNAPOTEZA WATEJA 10 KWA KUKOSA KITU HIKI.

Jifunze kwenye Kisa Hiki:

Kuna biashara moja ninaipenda sana kuifanya sasa nikawa nimejipa muda wa kutafuta jina zuri sana ili niisajili biashara ile. Siku moja nikapata jina zuri sana na nikalipenda.

Nikaingia kwenye mitandao ya kijamii kutafuta lile jina ili nione kama kuna mtu analitumia. Ukweli nikatafuta Instagram, facebook, google, sijaona mtu yeyote akitumia jina hilo.

Nikaamua kutengeneza kurasa za jina lile huku nikiwa na shauku kubwa sana maana nilipenda sana lile jina. Sasa baada ya kutengeneza majina yale nikaanza hatua za usajili wa jina lile.

Nikaingia kwenye tovuti ya BRELA (Hii ndio inayohusika na usajili wa majina ya Biashara hapa Nchini Tanzania) nikashtushwa sana kwa kukuta lile jina tayari kuna mtu amesajili. Nikaishiwa nguvu kabisa na ikanibidi nifute tu zile akaunti nilizotengeneza kwenye mitandao ya kijamii.

Nataka ujifunze nini kwenye mkasa huu ulionipata?

Kabla Hujasajili Jina la Biashara Yako Hakikisha Kwanza umefanya utafiti kidogo wa jina kuona kama tayari linatumika na mtu mwingine. Jina linaweza kutumiwa na mtu mwingine yeyote aliepo sehemu nyingine duniani mfano mimi ukoo wangu ni Mushi lakini ukiingia kwenye mtandao wa Google utaona Mushi.com ni tovuti inayomilikiwa na watu wengine ambao hata siwajui na wala sio watanzania.

Unapoona jina hakuna mtu anaelitumia basi usiishie tu kufurahi anza kulitumia wewe, tengeneza kurasa za mitandao ya kijamii, tengeneza website haraka sana kwani sio gharama kubwa sana kama ambavyo umekuwa unafikiri.

Hii itakusaidia kuwafahamisha wengine ambao wamewaza jina kama lako na wakaingia mitandaoni kutafuta kama jina linatumika basi wataona tovuti yako na kurasa za mitandao ya kijamii na hawataendelea tena na hatua nyingine.

Mimi ningekuwa mtu mbaya basi ningeweza kuingia Kenya na kulisajili lile jina na kisha kuendelea na kazi kama kawaida nikasajili website, na vitu vingine na tayari huyu aliekuwa amesajili Brela asingeweza kuendelea tena angebaki na vyeti tu vya usajili ingembidi atafute jina jingine la kujengea brand yake.

Mitandao ya Kijamii imeturahishia sana kujua nini kinaendelea sehemu zingine na kipi tayari kimeshafanyika au kinachofanyika. Usikubali tena kuishi kama zama zile ambazo hatujui kinachoendelea.

Kama mpaka sasa bado hujamiliki Tovuti kwa ajili ya biashara yako ni sawa na bado hujaimiliki biashara yako kwa asilimia zote.

Kila siku unapoteza wateja wengi sana ambao wanatafuta kile unachokifanya kwenye mtandao wa internet na kukukosa.

HATUA ZA KUSAJILI TOVUTI YAKO.

Tupatie Majina ya Biashara Yako

Tueleze Unataka jina gani (domain) mfano ni netpoa.com, netpoa.net

Sisi tunaangalia kama halijatumika bado halafu tunakusajilia kwa gharama nafuu sana.

Tuelezee Unataka Website Yako Iweje.

Tunakutengenezea Tovuti kwa namna ile ulivyotuelezea na ndani ya siku 7 inakuwa tayari hewani.

Kwa wewe  ambaye utawasiliana nasi leo utatengenezewa tovuti kwa punguzo la 30% (asilimilia thelathini) ya gharama halisi.

Wasiliana nasi leo kwa namba 0755 192 418

Bonyeza Maneno haya kuja Wasap wa.me/255755192418

KUMBUKA: TUNAKUSIKILIZA KILE UNACHOTAKA, NA KUKUSHAURI KILE KILICHO BORA.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *