Jinsi Ya Kutengeneza Mpesa VisaCard kwa ajili ya matumizi ya Mtandaoni.

Mpesa Visarcard ni nini? Huenda umejiuliza swali hili, nataka utambue kwamba kadiri tunavyoendelea kuwa na mabadiliko ya kiteknolojia kampuni ya mawasiliano ya simu ya Vodacom Tanzania wamekuletea fursa nzuri ya wewe kuuza au kununua bidhaa mtandaoni kwa kutumia Visacard yao.

Mpesa Visacard ni card ya kidigitali ambayo ipo kwenye mfumo wa tarakimu pekee na kwa kupitia tarakimu hizo utaweza kutumia mtandaoni kununua bidhaa kama ambavyo ungetumia card ya bank ya kawaida mfano Visa, na Visacard za bank nyingine.

Faida za Mpesa Visacard ni Zipi? Kwanini nitumie hii Mpesa Visacard na niache kutumia card nyingine?

Faida za Mpesa Visacard

Ni bure kuimiliki.

Ni rahisi kuwa nayo huhitaji vitu vingi kumiliki card hii ni simu yako tu.

Unatakiwa uwe na laini ya Vodacom Tanzania inayofanya kazi kwenye Mpesa. (yaani uwe una uwezo wa kuweka na kutoa pesa kwa Mpesa).

Haina gharama kubwa kwenye mtandao.

Unaweka ile pesa unayotaka kuitumia pekee.

Ni rahisi sana kuifuta na kutengeneza nyingine endapo umepoteza simu.

Ni rahisi kuweka na kutoa pesa zako, huhitaji ATM unaweka na kutoa kwa kupitia Mpesa yako.

Hizo ni baadhi tu ya faida nyingi ambazo utazipata ukiwa na mpesa Visacard endapo wewe unakuwa na matumizi mbalimbali kwenye mitandao kama kutangaza Facebook, Instagram, kulipia huduma zozote za kimtandao zinazokutaka uwe na card ya bank.

Jinsi ya Kutengeneza Mpesa VisaCard Yako.

Ingia kwenye Menu yako ya Mpesa yaani *150*00#

Chagua namba 4  Lipa kwa Mpesa.

Chagua namba 6 Mpesa Visacard

Chagua namba 1 Tengeneza Card

Nenda kwenye sms App uone card yako ya mpesa ya kidigitali.

Hizi namba ndio utakuwa unazitumia kuweka sehemu unapotaka kulipia huduma na wakataka utumie Visacard. Kuna Card namba (namba zilizo nyingi) kuna CVV (namba zilizo 3) na kuna Expire Date hii ni tarehe ya ku expire card yako ambapo utachukua mwaka na mwezi tu. Yaani mfano 2020/9/13 wewe utaweka mwezi 09/ mwaka 20.

Namba hizi zitunze sana kwasababu mtu akiziona anaweza pia kuzitumia kulipia chochote mtandao bila ya wewe kujua. Unaweza kuzihifadhi ili usije kuzisahau.

Hapo tayari unakuwa una Mpesa Visacard yako na utaweza kufuata utaratibu mwingine wa kuweka pesa kwenye card au kutoa pesa kwenye card na ni rahisi sana.

.

Kama una swali lolote usisite kutuandikia hapo kwenye maoni au unaweza kuwasiliana nasi kwa WhatsApp Bofya https://wa.me/message/M6OUG6EZ3KPAO1

KUMBUKA: NetPoa Hatutengenezi Mpesa Visacard, wala hatuna uhusiano wowote na kampuni ya Vodacom, sisi tunatoa elimu tu juu ya masuala yote yanayohusu Teknolojia.

Karibu Sana.

NetPoa Limited

1 reply

Trackbacks & Pingbacks

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply to NetPoa>Power Your Business to The World.>FAHAMU AINA 9 YA WATEJA KWENYE BIASHARA YAKO Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *