Jinsi Ya Kutengeneza Mpesa MasterCard kwa ajili ya matumizi ya Mtandaoni.

Mpesa Mastercard ni nini? Huenda umejiuliza swali hili, nataka utambue kwamba kadiri tunavyoendelea kuwa na mabadiliko ya kiteknolojia kampuni ya mawasiliano ya simu ya Vodacom Tanzania wamekuletea fursa nzuri ya wewe kuuza au kununua bidhaa mtandaoni kwa kutumia mastercard yao.

Mpesa mastercard ni card ya kidigitali ambayo ipo kwenye mfumo wa tarakimu pekee na kwa kupitia tarakimu hizo utaweza kutumia mtandaoni kununua bidhaa kama ambavyo ungetumia card ya bank ya kawaida mfano Visa, na Mastercard za bank nyingine.

Faida za Mpesa Mastercard ni Zipi? Kwanini nitumie hii Mpesa Mastercard na niache kutumia card nyingine?

Faida za Mpesa Mastercard

Ni bure kuimiliki.

Ni rahisi kuwa nayo huhitaji vitu vingi kumiliki card hii ni simu yako tu.

Unatakiwa uwe na laini ya Vodacom Tanzania inayofanya kazi kwenye Mpesa. (yaani uwe una uwezo wa kuweka na kutoa pesa kwa Mpesa).

Haina gharama kubwa kwenye mtandao.

Unaweka ile pesa unayotaka kuitumia pekee.

Ni rahisi sana kuifuta na kutengeneza nyingine endapo umepoteza simu.

Ni rahisi kuweka na kutoa pesa zako, huhitaji ATM unaweka na kutoa kwa kupitia Mpesa yako.

Hizo ni baadhi tu ya faida nyingi ambazo utazipata ukiwa na mpesa mastercard endapo wewe unakuwa na matumizi mbalimbali kwenye mitandao kama kutangaza Facebook, Instagram, kulipia huduma zozote za kimtandao zinazokutaka uwe na card ya bank.

Jinsi ya Kutengeneza Mpesa MasterCard Yako.

Ingia kwenye Menu yako ya Mpesa yaani *150*00#

Chagua namba 4  Lipa kwa Mpesa.

Chagua namba 6 Mpesa Mastercard

Chagua namba 1 Tengeneza Card

Nenda kwenye sms App uone card yako ya mpesa ya kidigitali.

Hizi namba ndio utakuwa unazitumia kuweka sehemu unapotaka kulipia huduma na wakataka utumie Mastercard. Kuna Card namba (namba zilizo nyingi) kuna CVV (namba zilizo 3) na kuna Expire Date hii ni tarehe ya ku expire card yako ambapo utachukua mwaka na mwezi tu. Yaani mfano 2020/9/13 wewe utaweka mwezi 09/ mwaka 20.

Namba hizi zitunze sana kwasababu mtu akiziona anaweza pia kuzitumia kulipia chochote mtandao bila ya wewe kujua. Unaweza kuzihifadhi ili usije kuzisahau.

Hapo tayari unakuwa una Mpesa Mastercard yako na utaweza kufuata utaratibu mwingine wa kuweka pesa kwenye card au kutoa pesa kwenye card na ni rahisi sana.

Hizi ni baadhi ya mifano ya vitu unavyoweza kulipia kwenye mtandao kwa kutumia Mpesa mastercard.

Kama una swali lolote usisite kutuandikia hapo kwenye maoni au unaweza kuwasiliana nasi kwa barua pepe support@netpoa.com

Karibu Sana.

NetPoa Technologies

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *