IFAHAMU DAWA YA KUVUTA WATEJA WAKUDUMU KWENYE BIASHARA YAKO.

Mimi Ninapenda sana maziwa ya mtindi, na hapa ninapokaa kuna duka ambalo huuza maziwa ya mtindi ya pakiti. Nimekuwa na mazoea ya kwenda hapo na kununua mara kwa mara ninapokuwa na hamu ya maziwa.

Siku za hivi karibuni nilikuwa nataka maziwa nikaenda, nikakosa nikazunguka sana hadi nikapata sehemu nyingine. Zikapita kama siku mbili tena nikahitaji maziwa nikaenda pale nilipozoea kununua nikakosa, jibu alilonipa ni kwamba leo hwajapitisha. Nikazunguka tena hadi nikapata kwenye duka lile lile nililonunua juzi.

Mara nyingine ya tatu nikaenda tena pale nilipozoea nikakosa, sababu ilikuwa ni ile ile. Nikaenda kule niliponunua juzi. Sasa leo nimesikia hamu ya maziwa nikataka kwenda pale kwa jirani akili ikaniambia unweza kukuta hana ukajisumbua bure.

Nikaamua kwenda zangu kule nilipoenda kwa siku tatu nikapata maziwa ya uhakika.

Huyu jirani yangu hapa ninaweza  nisiende tena kununua hata vitu vingine niende kule mbali kabisa kwasababu nahisi atakuwa hana. Hata nataka kununua mtindi Pamoja na unga ni bora niende kule mbali ninunue vyote kwasababu ni uhakika.

Sasa Rafiki kuna nyakati unaweza kufikiri umelogwa kumbe hakuna aliekuloga, unaweza kufikiri jirani yako anatumia madawa kumbe hapana, wewe ndio una matatizo. Unawasumbua wateja wako bure. Kila siku anakuja akihitaji huduma anakuta haipo. Lazima mteja atakuhama.

Kuna njia moja ya kuhakikisha wateja wako wanakupata wakati wote wanapokuhitaji. Hata kama umefunga ofisi yako, ipo njia ambayo wateja wakihitaji kuifahamu biashara yako hata usiku wa manane wanaweza kuifahamu bila hata ya kukusumbua uwaelezee.

Unaweza kuwa na ofisi nzuri sana, na bidhaa/huduma bora na nzuri sana lakini ukakosea kitu kimoja tu. Wewe unapofunga jioni Pamoja na wenzako, wewe ndio unakuwa umefunga kumbe wenzako biashara zao hawajazifunga bado zipo wateja wakihitaji kuona bidhaa au huduma wanaweza kuziona wakati wowote.

Kuna wateja wanakuja kwenye biashara yako nyakati ambazo wewe tayari umefunga hawa wanakupataje? Waende warudi kesho? Haupo makini na biashara yako kweli, labda kama ni wewe tu unaefanya hiyo biashara hapa mjini.

Unawapoteza wateja wengi sana ambao hawawezi kufika kwenye ofisi yako kwasababu wapo makazini mwao. Unawapoteza wateja wengi sana ambao hawakujui lakini wanahitaji kile unachouza.

Ipo njia moja na rahisi sana lakini yenye matokeo makubwa mno. Njia hii ni kuwa na TOVUTI (WEBSITE). Hii ndio njia pekee ya kukusaidia wewe kufungua biashara yako Masaa 24 hata kama umelala. Tovuti ndio ofisi yako ya kidigitali ambayo haikuhitaji wewe uwepo.

NetPoa Tunatengeneza Tovuti za Kisasa ambazo mteja akitembelea lazima avutiwe na zile huduma au bidhaa unazotoa na kufanya malipo.  Hamia sasa kwenye ulimwengu wa kidigitali kwa kufungua tovuti ambayo itakufanya ufanye kazi masaa 24 hata wakati ambao umelala.

Wasiliana Nasi Leo Tukutengenezee Tovuti Ya Biashara Yako. Usikubali kuendelea kupoteza wateja wako wa muhimu wanaotamani kuja ofisini lakini hawawezi.

Wasiliana Nasi Sasa.

Wasap 0755 515 122

Barua pepe jacob@netpoa.com

Tovuti www.netpoa.com

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *