Jinsi ya Kubadili Ukurasa wa kawaida wa Facebook Kuwa wa Biashara.

Karibu kwenye mtandao wa netpoa.com leo tumekutana tena kuzungumzia teknolojia.

Inawezekana umekuwa unataka kufungua kurasa facebook kwa ajili ya biashara yako na ukaanza kuona imekuwa kazi kubwa sana kuukuza ukurasa huo kuanzia sifuri.

Makala ya leo inakwenda kukupa njia za kukuwezesha uweze kutengeneza ukurasa wa biashara ukiwa na wale mafriends zako kwenye ukurasa wa kawaida.

Twende pamoja mpaka mwisho uweze kujifunza na unufuaike kwenye biashara yako leo.

Tuangalie Faida za Kuwa na Ukurasa wa Biashara wa Facebook.

  • Unapata Nafasi ya Kutenganisha Ukurasa Binafsi na Biashara.
  • Unapata Nafasi ya Kuendesha Ukurasa huo kwa kutumia akaunti ile ile moja.( Ukisema ufungue account mpya kwa ajili ya biashara maana yake utakuwa una logout na ku login kila wakati ili uweze kuzitumia zote au itakugharimu kutumia vifaa viwili tofauti)
  • Unapata Nafasi ya wateja au watu wanaopenda biashara yako kukufuata tu na sio wewe tena kuwafuata. (Ukurasa wa kawaida unakulazimisha uwaombe urafiki wengine)
  • Unapata nafasi ya kuwa na watu wengi bila ya kikomo. (Ukurasa wa kawaida marafiki wanaishia elfu tano tu, na itakupasa uweke uwezo wa watu kukufuata)
  • Hupati kazi ya Kukubali Urafiki wa kila mtu kama akaunti ya kawaida.
  • Unapata nafasi ya kuunganisha na Instagram yako
  • Unapata Nafasi ya Kutangaza kwa Kulipia na kuwafikia watu wengi.(ukurasa wa kawaida hauna uwezo wa kulipia matangazo)

Hizo ni baadhi ya faida nimekutajia hapo na utaweza kuona kwamba zipo nyingi sana.

Sasa twende kwenye lengo la makala yetu ya Leo, unawezaje kutengeneza ukurasa wenye wale marafiki wako kwenye ukurasa wa kawaida? Ni rahisi sana, mimi nitakuwekea link hapa utaibonyeza na utafuata maelekezo na mwishoni kabisa utaona umekuwa na ukurasa wenye idadi ile ile ya marafiki na watu walio ku follow (kufuata).

Bonyeza Hapa kubadilisha Facebook ya Kawaida na Kutengeneza Ukurasa wako wa Biashara. www.facebook.com/pages/create/migrate N.b ili upate matokeo utapaswa kubonyeza link hii kwenye computer, kwenye simu hutaweza kuhamisha wale marafiki.

Kama unatumie ukurasa wa Facebook Bonyeza Hapa ulike ukurasa wetu wa netpoa www.facebook.com/netpoaltd

Kwa Uhitaji wa Blog, na Website Tembelea hapa www.netpoa.com

Je Una swali lolote? Andike kwenye comment nitakujibu.

Karibu Sana.

1 reply

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *